Wakazi wa Kijiji cha Wembere na vitongoji vyake wilayani Iramba mkoani Singida wameiomba serkali kuwasaidia kutatua changamoto ya miundombinu ya jamii hususani barabara ambayo haipo katika hali nzuri kutokana na mito mikubwa kukatika bila ya uwepo wa madaraja
Wameyabainisha hayo wakati tume ya Taifa ya Matumizi Bora ya Ardhi ikikamilisha uandaaji wa matumizi bora ya ardhi katika vijiji 48 vya halmashauri tatu za mkoa wa Singida na kubaini changamoto za ubovu wa miundombinu ya huduma mtambuka za jamii kuwa kikwazo.
Na JAMALDINI ABUU
Katika wilaya ya Iramba mojawapo kati ya wilaya Tano za mkoa wa Singida, kuna kijiji kinaitwa Wembele Miongoni mwa kijiji kati ya vijiji 70 vya wilaya hio, kijiji kinachopatikana chini ya milima ya Sekenke katika Tarafa ya Shelui
Safari ya masaa takribani mawili na nusu kutoka katikati ya mkoa wa Singida (Manispaa ya Singida) imenifikisha na kunikutanisha na wakazi wa kijiji hiki wanaonisimulia wanayoyapitia katika maisha yao ya kila siku
Wakazi hawa wanaoishi kwa kutegemea kilimo na ufugaji kuendesha maisha yao wanasema changamoto ya miundombinu ya huduma za kijamii kutokuwepo ama kuchakaa kwao imekuwa kikwazo katika maisha yao ya kawaida

Kaimu mwenyekiti wa kijiji hiko Haruna Abubakari amesema miundombinu hasa barabara haiko sawa na hata shule imeshachakaa kutokana na mindombinu yake kuwa ni miaka mingi
“Mimi namuomba mama Samia atuangalie kwanza shule imeshakuwa mbovu mana ni toka enzi za mkoloni imeshachakaa lakini barabara tunahangaika na mto ule Kibigili na hata mwanamke akipewa rufaa kwenda hospitalini kuvuka pale inakuwa shida tunaomba tuwekewe daraja” alisema
Nae Katalina Deogratius mkazi wa kijiji hiko cha Wembere anasema anasema kwasasa wanafunzi wa sekondari wanatembea umbali mrefu kufika shuleni na kutamani kupata shulke ya sekondari karibu kupunguza umbali wa kutembea kwa watoto wao
Samson Mkabila mkazi wa Kijiji hiki anasema wao kama wakazi wa kijiji hiko wanahangaika kutafuta malisho ya wanyama wao kwakuwa awali walikuwa wakichunga mlimani kabla ya serikali kujakuzuia milima hiyo kuwa hifadhi msitu na kuweka katazo la uchungaji
Ameiomba serikali kuimarisha miundombinu ya barabara na kuwatengea maeneo ya malisho ya mifungo ili kupunguza kuhangaika
“hifadhi hii ndio tulikuwa tunaitegemea kwa wananchi wa kijiji cha wembere kulishia wanyama”
Serikali katika kuhakikisha inatatua changamoto za wananchi nchini, Tume ya Taifa ya Matumizi Bora ya Ardhi imekamilisha zoezi la uandaaji wa matumizi bora ya ardhi katika vijiji 48 vya halmashauri tatu za mkoa wa Singida ikiwemo kijiji cha Wembere licha ya kubaini changamoto za ubovu wa miundombinu ya huduma mtambuka za jamii kuwa kikwazo kwa wakazi wa vijiji hivyo
Zoezi hilo lililofanyika kwa Miezi Mitatu limetekelezwa katika halmashauri za wilaya ya Manyoni, Ikungi na Iramba huku kila halmashauri katika hizo zikifikiwa vijiji 16 nakujumuisha vijiji 48




