Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego amewataka wazazi na jamii kwa ujumla kuhakikisha malezi ya msingi kwa Watoto yanatokana na misingi ya dini, mila, desturi na tamaduni kutokana na baadhi ya watu wanaofungwa gerezani kutamani kurudi tena gerezani baada ya kutoka na kupelekea kujihusisha katika vitendo uhalifu
Hayo ameyasema wakati akizundua BODI YA PAROLE katika ukumbi wa Ofisi za Magereza Mkoa nakuhudhuriwa na wajumbe wa Bodi, Kamati ya Ulinzi na usalama mkoa, pamoja na Sekretarieti
Dendego amesisitiza elimu kutolewa kwa wananchi ili kuelewa kwa undani zaidi kuhusu majukumu ya Bodi ya Parole na umuhimu wake kwa walengwa wa moja kwa moja ili kuendelea kunufaika na fursa hiyo
“wazazi warudi katika majukumunyao ya msingi ya kulea Watoto,tusiache nafasi kubwa kwa Watoto kujifunza katika mifumo kama mitandao ya kujamii, bali tuwale katika misingi ya dini,mila, desturi na tamaduni zetu” amesema Dendego
Kwa upande wake mwenyekiti wa Bodi hiyo mkoa wa Singida Liana Hassan ameahidi kushirikiana na Ofisi ya mkuu wa mkoa, menejimenti, Katibu wa Bodi na timu yake katika kutekeleza kazi huku akisisitiza utayari katika kufanya kazi na ushirikiano baina yao kwa maslahi mapana ya Jeshi la Magereza na Taifa kwa ujumla
“Tutatoa ushirikiano mkubwa katika utekelezaji wa kazi hii ambayo tumeaminiwa kuifanya,tuwe na utayari kufanya kazi ambayo Serikali yetu imetuamini kuifanya”Alisema Liana
Nae katibu wa Bodi hiyo ambaye ni mkuu wa Magereza Mkoa wa Singida SACP Khatibu Semzono mpaka sasa takribani wafungwa 218 wamenufaika na bodi hiyo tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 2003 huku bodi hiyo ikikabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo jamii kuwa na elimu ndogo kuhusu wafungwa wanaoachuliwa kwa mpango wa Parole, ikiwemo na jamii kutotoa ushirikiano hasa kwa waathirika
NB: Asante kwa kuendendelea KUTUAMINI na KUTUFUATILIA🙏 KAJEM TV NA BLOG YETU YA KAJEMEDIA NA MITANDAO YETU YA KIJAMII ipatikanayo kama KAJEMTV. Maoni Yako ni ya msingi sana kwetu kwani KAJEM TV #Tunakuzingatia. Wasiliana nasi Sasa kupitia Namba 0626007143 pamoja na mitandao yetu ya kijamii
#kajemtv #news #sisinawewe #tunakuzingatia #kajem









