SINGIDA KUWA NA TIMU MBILI LIGI KUU, YATENGWA MILIONI 67

Shirikisho la mpira wa miguu mkoa wa Singida (SIREFA) limeweka bayana nia ya kutaka kuwa na timu mbili zinazoshiriki ligi kuu ya Tanzania bara (NBC Primer League) kwa msimu wa mwaka 2025/2026

Hayo ameyasema mwenyekiti wa SIREFA Hamisi Kitila Katika Mkutano mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu mkoa wa Singida (SIREFA) uliofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Singida leo jumamosi ya August 17,2024
Kitila amesema kwasasa mkoa unafaidika na uwepo wa timu moja iliopo hivyo wanatarajia kuongeza timu nyingine kwaajili ya manufaa zaidi ya kimkoa na shirikisho 

"Tunataka mwakani kupata timu nyingine ya ligi kuu kwa kushirikiana na wadau wengine, kwasasa wananchi wa mkoa wa Singida wanapata burudani lakini pia uchumi unaimarika" 

Singida Black Stars ndio timu pekee kwasasa inayoshiriki ligi kuu kwa mkoa wa Singida mara baada ya kubadilishwa jina kutoka Ihefu baada ya kuhamia kutoka mkoani Mbeya kuja mkoa wa Singida na Singida Fountain Gate kuhamia mkoa wa Manyara na kubadilishwa jina kuwa Fountain Gate fc

Kwa mujibu wa mhasibu wa SIREFA Charles Kimwaga amesema kwa mwaka huu shirikisho limetenga bajeti ya milioni 67 ikiwa na ongezeko la milioni 17 toka bajeti ya mwaka Jana ambayo ni milioni 50
"Kwa mwaka huu tumetenga bajeti ya milioni 67" amesema mhasibu Kimwaga

Mkutano huo ulikuwa na dhima ya kufanya uchaguzi kwaajili ya kupata uongozi mpya wa shirikisho utaongoza kwa mwaka wa 2024/2025 ambapo katika nafasi ya mwenyekiti, makamo mwenyekiti nafasi hizo zilikuwa na wagombea mmoja mmoja ambao wote walipita 

Katika uchaguzi huo Hamisi Kitila amechaguliwa tena kuwa mwenyekiti wa SIREFA kwa miaka 4 ijayo akipigiwa kura zote 13 za wajumbe wote walioshiriki huku Yagi Maulid Kiaratu (Meya wa manispaa ya singida) akichaguliwa kwa kura zote 13 kuwa mjumbe wa kamati kuu ya TFF


Post a Comment

Previous Post Next Post