LAMECK LAWI MARA HII ATUA AZAM FC, ASAINI MIAKA 2 BAADA YA KUIKOSA SIMBA MSIMU ULIOPITA

Lameck Lawi alianza kusikika akiwa mlinzi wa Coastal United ya Tanga, nakuisaidia timu hiyo kufikia nafasi ya nne uliopita na kushiriki Kombe la Shirikisho Barani Afrika 2024/25

Lawi aliwavutia Miamba ya Soka Nchini Simba SC, Yanga SC na Azam FC kutokana na uwezo wake Katika Msimu wa 2023/24, na Coastal Union walithibitisha kupokea ofa kutoka klabu hizo

Mnamo Juni 2024, Simba ilitangaza kumsajili Lameck Lawi kwa mkataba wa miaka mitatu kwa Dau la Sh. 230 m, na akatambulishwa rasmi kabla coastal kukataa kuidhinisha uhamisho kutokana na Simba kutofuata taratibu za malipo ya usajili ndani ya muda ulioafikiwa

Lameck Lawi Mnamo Julai 2024, Alifanya vipimo vya majaribio katika Klabu Ya K.A.A. Gent (Ligi ya Ubelgiji) na kuendelea na mazoezi Katika Klabu Hiyo Na Baadae Lameck Lawi alirejea Coastal na akawa mmoja wa nguzo zao, akishiriki kikamilifu msimu 2024/25 katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara

Lameck Lawi ni kifaru kipya kilichotokea katika Ligi Kuu ya Tanzania mzuri kimwili, na mwenye hamu kubwa ya kukua na kwenda nje ya nchi. Ingawa akaona changamoto za usajili

Msimu huu umekuwa changamoto kwake na kwa Coastal Union, wakishuka hadi nafasi ya 9 kati ya timu 22, lakini Lawi ameonyesha mtazamo wa kujifunza na kuimarika kikosi mpaka mwisho na Rasmi Amesinya Miaka 2 Kuwatumikia Wanalambalamba Wa Azam Fc



Post a Comment

Previous Post Next Post