MWENGE WA UHURU WATIA KAMBI SINGIDA, MIRADI YA ZAIDI YA BIL. 62.6 KUGUSWA

Miradi yenye thamani ya zaidi ya Sh.Bilioni 62.6 iliyojengwa katika halmashauri saba za zilizopo katika Mkoa wa Singida itazinduliwa na kukaguliwa na Mwenge wa Uhuru 2025 ambao utakimbizwa kwa siku saba mkoani hapa.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, akitoa taarifa jana kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka huu, Ismail Ally Ussi, baada ya kuupokea katika kijiji cha Sagara Halmashauri ya Wilaya ya Singida ukitokea Mkoa wa Manyara.

Alisema katika miradi hiyo mchango wa serikali kuu ni asilimia 92,asilimia 6.7 wahisani, halmashauri asilimia 1 na wananchi ni asilimia 0.2.

Dendego alisema Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Mkoa wa Singida utakimbizwa jumla ya kilometa 842.6 katika halmashauri zote saba za mkoa huu na kwamba kila eneo wananchi wamejipanga kuupokea.

Akizungumzia kuhusu uchaguzi Mkuu unaitarajia kufanyika Oktoba mwaka huu alisema mkoa umejipanga vizuri ambapo asilimia 99.6 ya wananchi wa Singida wamejiandikisha kwa ajili ya kushiriki uchaguzi huo.

Katika mbio zake mwenge umezindua Mradi wa maji katika kijiji cha kinyamwenda katika Tarafa ya Mgori,Kata ya Itaja unaogharimu kiasi cha shilingi 955,205,436.75 kutoka serikali kuu umekamilika kwa asilimia mia moja (100) kupitia mpango wa Lipa kulingana na Matokeo yaani

Mradi huu unajumuisha ujenzi wa tangi la maji lenye uwezo wa kubeba lita 100,000 kwenyenara wa mita sita pamoja na uzio,ujenzi wa vituo vya kuchotea maji 12,ujenzi wa mrambo wa kuchotea mifugo,mtandao wa mabomba yenye urefu wa km 14.6,na mfumo wa nishati ya jua kwa ajili ya kuendeshea pampu

Mradi huu una pampu yenye uwezo wa kutoa lita 13,500 kwa saa utawanufaisha wananchi zaidi ya 3134 wa Kinyamwenda,kadhalika mifugo 4175 kwa kupata maji safi na salama

Imeandikwa Na Thobias Mwanakatwe

 

 

Post a Comment

Previous Post Next Post