TANESCO SINGIDA YAMKAMATA MTUHUMIWA WA WIZI WA UMEME, ATUMIA BILA KULIPIA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani Singida limeanza Oparesheni maalum ya kuwasaka na kuwachukulia hatua kali wanaojihusisha na uharibifu wa miundombinu ya umeme pamoja na wizi wa nishati hiyo

Katika utekelezaji wa Operesheni hiyo Mtaa wa Minga manispaa ya Singida imemkamata  Ashura Athumani mkazi wa mtaa huo kwa wizi wa umeme kwa kujiunganishia mojakwamoja bila kupitia kwenye Mita hivyo kutumia bila kulipia

Kwamujibu wa Mdhibiti Mapato wa TANESCO Mkoa wa Singida, Mhandisi Lugano Mwakinyala, amesema oparesheni hiyo inalenga kukomesha vitendo vya wananchi kujiunganishia umeme kinyume cha taratibu kwa kutumia mafundi wasio rasmi na kuongeza kuwa hatua wanayochukua kwa Mwizi huyo ni kumjazisha fomu ya ukaguzi na kumkatia umeme kwakuwa Mita iliyotumika hawaitambui


Kwa upande wake
Ashura Athumani ameeleza kutotambua chochote kutokana na wizi huo kwakuwa wao wamepangisha eneo hilo tangu mwaka jana (2024) mwezi wa tisa na kuikuta mita hiyo bila kujua kama ni ya wizi au laa

"Opararesheni hii inalenga kukomesha wizi na hii nyumba tunaondoa huduma hii kwakuwa hii mita hatuitambui," Lugano

Aidha kwa upande wa udhiniti mapato Augustino Shirima amesema kuaa waliounganisha umeme katika nyumba hiyo wametumia mbinu ambazo umeme unaingia moja kwa moja hausomi katika mita ambayo imefungwa.

Ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kutumia huduma rasmi ya Nikonekt ya TANESCO ili kupata maombi ya umeme kwa njia salama, rahisi na ya haraka, badala ya kutumia njia zisizo halali ambazo huweka maisha na mali zao hatarini.


Shirika hilo limeahidi kuendelea na oparesheni hiyo katika wilaya zote za Mkoa wa Mwanza hadi vitendo vya hujuma na wizi wa umeme vita kapokoma kabisa.



Post a Comment

Previous Post Next Post