KARIA 100% URAIS TFF AWAMU YA TATU, WAJUMBE WOTE WAMPIGIA KURA BILA KUKATALIWA HATA NA MMOJA

Wallece Karia ameidhinishwa kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Kwa kupigiwa kura na wajumbe wote 76 wa mkutano mkuu wa TFF Jijini Tanga
Hayo Yamejiri Hii leo Jumamosi ya Agosti 16, 2025 ambapo Karia amepita baada ya Wajumbe Kunyoosha mikono ya kumuidhinisha bila kupingwa hata na Mjumbe Mmoja

Karia alikuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo baada ya wagombea wengine kuenguliwa kwa kukosa vigezo vya kikanuni

Karia amekuwa Rais wa TFF Tangu Mwaka 2017 akichukua nafasi hiyo kutoka kwa mtangulizi wake Jamal Malinzi na kisha kutetea nafasi hiyo mnamo Agosti 7, 2021 kwa awamu ya pili kwa kupigiwa kura zote 81 kabla ya leo kupitishwa tena kuwa Rais wa TFF kwa awamu ya Tatu

Tangu mwaka 2019 alihudumua kama Rais wa Jumuiya ya Mashirikisho ya Mpira wa Miguu ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) na mnamo Machi 2025, aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF Executive Committee), akiwakilisha eneo la CECAFA

Post a Comment

Previous Post Next Post