SIMBA DAY MKALAMA YASHEHEREKEWA KWA MKONO WA FARAJA KWA WENYE MAHITAJI

Na Mwandishi Wetu

Mkalama, Septemba 6, 2025 – Mashabiki wa Klabu ya Simba kutoka Wilaya ya Mkalama wameadhimisha Simba Day kwa kugusa maisha ya watu wenye mahitaji kwa kutoa misaada mbalimbali.

Misaada iliyotolewa ilihusisha taulo za kike kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mkalama One, pamoja na mahitaji kwa akina mama (wazazi) waliolazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mkalama na kusaidia kaya zisizo jiweza 

Akizungumza wakati wa tukio hilo, Mratibu wa zoezi la Simba Day Wilaya ya Mkalama, Mwalimu Simon Molel, aliwapongeza mashabiki wa Simba kwa moyo wa kujitolea na kujali makundi yenye uhitaji. Pia alihimiza jamii kuendeleza utamaduni wa kusaidiana mara kwa mara kama njia ya kujenga mshikamano.


Post a Comment

Previous Post Next Post