Kwa Mujibu wa taarifa iliyotolewa na club hiyo inasema kuwa kifo cha Manji kimetokea hii leo 30 June, 2024 katika nchi ya Marekani ambapo Alikuwa akipatiwa matibabu ya maradhi yaliokuwa yanamsumbua
Kwa Mujibu wa Eng. Hersi Said ambaye ni Rais wa Yanga kwasasa amemtaja Manji kama kiongozi hodari na mahiri aliyejituma na kujitoa kwaajili ya maendeleo ya timu yao, na kusema kuwa kifo chake ni pigo kwa wanayanga na familia nzima ya michezo
“Manji alihudumu katika nafasi Mbalimbali za kiungozi ndani ya club yetu kama mdhamini na Mwenyekiti ambapo hadi umauti unamkuta alikuwa mwanachama na Young Africans Sports Club, uongozi wa Young Africans Sports Club unatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wanamichezo wote nchini kwa msiba mzito wa mpendwa wetu”


