SUWASA Yaelezea Maendeleo Ya Mradi Wa Majitaka, Bil. 1.7 kutumika kutekeleza

Na Jamaldini Abuu

Singida

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) imetoa elimu kwa wananchi wa eneo la Manga kuhusu maendeleo ya Ujenzi wa Mradi  wa Mabwawa ya Kutibu Majitaka Manga.



Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa SUWASA Hosea Maghimbi amewashukuru wananchi na Serikali ya kijiji cha Manga kwa kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa mradi huo tangu ulipoanza huku akibainisha kuwa mradi huo unatarajia kugharimu kiasi cha sh. 1.7 bilioni kutoka serikali kuu


Hosea amebainisha kuwa mradi kama huo wa maji taka ni mradi wa kwanza kutekelezwa kwa mkoa wa singida hivyo wananchi hasa waishio jirani na mradi huo watanufaika hasa kwa kilimo cha mbogamboga kutokana na maji yatakayotokana na mabwawa hayo






katika hatua nyingine SUWASA imetoa vyeti vya shukrani kwa wananchi waliotoa maeneo yao kupisha utekelezaji wa mradi huo, vyeti ambavyo vilikabidhiwa kwa wananchi hao na Diwani wa Kata hiyo ya Mtipa Mhe. Ramadhani Said 

Mhe. Diwani amewasihi wakazi wa kata ya Manga kuendelea kupokea na kufurahia Miradi ya Maendeleo ili kata ya Mtipa iweze kuendelea kwa haraka zaidi na kusema mradi huo umewawezesha wakazi maeneo ya jirani kupata ajira za muda kupitia utekelezaji wa mradi huo




nao baadhi ya wananchi waliojitokeza kupata elimu juu ya mradi huo wameonyesha kufurahishwa mno na uwepo wa mradi huo huku wakisema uwepo wa mradi huo utawainua kiuchumi kutokana na kilimo cha mbogamboga na umwagiliajai


Kwa upande wake Abubakar Msamaha mkazi wa kijiji cha Manga amesema manufaa watakayoyapata kutokana na mradi huo ni pamoja na kilimo cha umwagiliaji huku Juma Mohammed mkazi wa kijiji hiko akisema mradi huo umeondoa adha ya maji katika kijiji chao 

"manufaa ni kwa kilimo cha umwagiliaji pamoja na mbolea kutoka kawenye hayo maji, watu watalima mbogamboga watapata hela" alisema Juma

Post a Comment

Previous Post Next Post