HISTORIA YAANDIKWA KANISA KATOLIK JIMBO LA SINGIDA LIKIFANYA UPADIRISHO WA MAPADRE 10 NA SHEMASI KWA PAMOJA

Kanisa katoliki jimbo kuu la Singida limeandika historia mpya marabaada ya kufanyika maadhimisho ya Upadirisho kwa Mapadre 10 na Shemasi mmoja ikiwa ni kwa mara ya kwanza tukio kama hilo kufanyika katika historia ya jimbo hilo

Maadhimisho hayo yakuwekwa wakfu yamefanyika June 27,2024 katika ukumbi wa kanisa katolik jimbo kuu la Singida huku ikielezwa kuwa tukio kama hilo linalojumuisha Mapadre na Mashemasi katika tukio moja ni nadra kutokea

Askofu wa kanisa katolik Jimbo la Singida Askofu Edward Mapunda akiwapa Upadirisho Mapadre 10 katika ukumbi wa kanisa katolik Jimbo la singida

Mapadre hao 10 waliopatiwa Upadirisho wanajumuisha Mapadre 8 wa jimbo na wawili wa mashirika huku mara ya mwisho Upadirisho kama huo kufanyika ukijumuisha idadi kubwa ya Madapre ni mwaka 1993 ambapo takriban Mapadre 5 walipatiwa Upadirisho

Akizungumza wakati akiwapa Upadirisho huo baba Askofu wa jimbo hilo Askofu Edward Mapunda amewataka mapadre hao kwenda kutangaza upendo na amani na kuwatumikia masikini na watu wote wananowazunguka bila ubaguzi

Askofu wa jimbo hilo Askofu Edward Mapunda akizungumza na hadhara iliyojitokeza katika Warsha hio ya Upadirisho

Aidha Askofu Mapunda amesema nafasi walioipata ni zawadi kutoka kwa Mungu na amewataka waende wakafundishe dini katika shule ngazi zote na vyuo kutokana na kile alichokisema kama shida kubwa ya kutofundishwa kwa dini shuleni

“Nendeni mkafundishe dini shule za msingi, shule za sekondari, na kwenye vyuo, kila mmoja aende akafundishe dini huu ndio utume wenu namba moja na hiki kiwe kimbaombele chenu, kuna shida kubwa huko shule nyingi dini haifundishwi kwahiyo nyinyi mkafundishe dini” alisema Askofu Mapunda


Askofu wa jimbo hilo Askofu Edward Mapunda akizungumza na Mapdre 10 na Shemasi kuwapa somo katika utumishi wao mara baada ya Upadirisho

Katika hatua nyingine amewataka waende wakaishi maisha ya kawaida yasio ya gharama huku akiwataka waene wakajiepushe na mambo ya biashara ambayo yanaweza kupunguza ufanisi katika utumishi wao kwamana wao jukumu lao sio kufanya biashara bali ni kuokoa roho za watu

“Padre ni daraja kati ya mungu na wanadamu kwa njia ya utumishi wake wa neon na kwa njia ya sakrament mbalimbali, padre ni mhudumu wa neo la mungu na sakrament takatifu na upadre ni zawadi kutoka kwa mungu na kanisa lake” alisema




Maadhimisho hayo yamehudhuria na mamia ya wafuasi wa dhehebu hilo kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Singida na mikoa mingine ikiwemo Dodoma, Manyara na Mbeya na kuhudhuriwa pia na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa na serikali pamoja na Maaskofu wa majimbo ya Mbeya na Dodoma



Tukio hilo limeambatana na kilele cha Jubilei ya miaka 50 ya Jumuiya ndogondogo ambayo nayo ilijumuishwa katika maadhimisho hayo



Post a Comment

Previous Post Next Post