Kupitia harambee iliofanyika june 30, 2024 katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya kati Singida takribani kiasi cha sh. milioni 800 zimekusanywa ikiwa ni ziada ya milioni 100 kutoka kwenye kiasi kilichotarajiwa
Katika harambee hii ya pili iliyokusudiwa kukusanya kiasi
cha milioni 700 ziada ya milioni 300 kutoka kwenye harambee ya mwaka jana
iliyokusanya kiasi cha milioni 400 kwa lengo la kwenda kuimarisha vituo vya afya,
shule na mfuko wa utumishi
Akizungumza kwaniaba ya mgeni rasmi, Prof. Kitila
Mkumbo amewataka wananchi wawe na desturi ya kujitolea ili waongezewe zaidi
kama ambavyo maandiko yanasema
Kwa mujibu wa askofu Dr. Syprian Hilinti amesema
harambee ya mwaka huu imekusudia kukusanya milioni 700 ili kwenda kuimarisha
vituo vya elmu Ihanja na Kiomboi pamoja vituo vya afya Singida Mjini na Iyambi
na kuinua mfuko wa utumishi
“Dayosisi yetu tumejiwekea nadhiri kwa mungu na
patano kupitia vikao vya kimaamuzi na kikatiba kwamba kila mwaka kila msharika
kuanzia mtoto hadi mzee atamuwekea mungu alama kwa mchango wake wa sadaka ya
hiari na moyo wa kupenda kama mungu anavyomuongoza”
Kwa upande wake mkuu wa kanisa Tanzania Alex
Malasula amewataka vijana nchini kujielekeza maisha yao kwa mungu ili kudumisha
amani kwani amesema endapo vijana wakijielekeza kwa mungu chochote
atakachokifanya atamuuliza mungu kabla ya kutenda hivyo nchi itakuwa mahali
amani
“kijana akiweka maisha yake kwa mungu nchi yetu
itakuwa mahali pa amani, nchi yetu itakuwa mahali penye ufahamu, kijana
aliyeweka maisha yake mahali pa mungu anaufahamu kabla hata ya kuamua lolote
anamuuliza mungu”
Katika harambee hio imehudhuriwa na viongozi
mbalimbali kutoka madhehebu tofauti ya dini tofauti, viongozi wa serikali ngazi
tofauti, viongozi wa vyama vya siasa, wabunge mbalimbali wa mkoa wa Singida,
huku mgeni rasmi akiwa waziri wa fedha Dr. Mwigulu Nchemba akiwakilishwa na
waziri wa mipango na uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo
Mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dendego amesema
serikali ya mkoa wa Singida inaushirikiano mzuri na madhehebu ya dini katika
kuendeleza maendeleo ya mkoa na ndiomana tukio hilo la kikanisa limejumuisha
watu wa hadhi na imani tofauti
“Na hizifedha zinazochangwa zinaenda kutoa mchango
mkubwa kwenye elimu na afya, kila mmoja wetu ataguswa moja kwa moja kupitia
ndugu yake, mdogo wake, kakayake, rafikiyake, mtoto yake au mgeni wake, kwahiyo
hili jambo ndugu zangu ni lakwetu sote” alisema



