Ni mshambuliaji raia kutoka nchini Uganda, aliyejiunga rasmi msimbazi kuwafuta machozi ya muda mrefu mashabiki na wanachama wa Simba kwenye ule mfupa uliowashinda baadhi ya washambuliaji kwa miaka ya hivi karibuni wakiwemo kina Jeneral Mosses Phiri, na Jean Baleke,
Steve Mukwala mwenye umri wa 20 na Minne,
mshambuliaji kinara aliyefunga mabao 14 na usaidizi wa magoli mawili katika
michezo 28 akiwa na Asante Kotoko ya nchini Ghana msimu uliomalizika, anasaini miaka
3 kuitumikia nembo ya Simba
Ni Mukwala Mwenye urefu wa futi 5.9 amebeba
matumaini ya wanamsimbazi kutibu moja ya eneo lililokuwa na mapungufu makubwa msimu
uliomaliza katika kikosi hiko, eneo la safu ya ushambuliaji, anakuja kuungana
na Fredy Michael kuiongoza safu hio
Steve Mukwala katika historia yake ya kabumbu
amevitumikia vilabu kadhaa nchini Uganda ikiwemo Vipers Fc, Maroons Fc kabla ya
kutimkia Asante Kotoko ya nchini Ghana
Licha ya kufunga magoli 14 msimu uliopita, msimu wa
mwaka juzi alipachika magoli 11 pekee katika michezo 31 aliyocheza ya ligi
Siku moja kabla ya kutambulishwa Mukwala pale
msimbazi, alitambulishwa mchezaji raia wa Zambia Joshua mwana wa Mutale, kiungo
mwenye umri wa miaka 22 aliyejiunga na Simba kwa mkataba wa miaka 3 akitokea Power
Dynamo ya nchini Zambia
Ni Joshua Mutale anayeweza kucheza akitokea kulia,
kushoto ama kucheza nyuma ya mshambuliaji kama namba 10
Mutale Akiwa Zambia na Power Dynamo msimu uliopita
amefunga magoli 8 katika michezo 26
aliyocheza
Mpaka sasa
simba imeshatambulisha wachezaji 3 waliowasajili katika kikosi chao nje
na walioongezewa mkataba. Mapema kabisa alitambulishwa Lameck Lawi kutoko kwa
wanamangushi, Costal Union ya mkoani Tanga anayecheza nafasi ya mlinzi wa kati,
kisha kiungo Joshua Mutale na baadae mshambuliaji Steve Mukwala



