MGANGA WA KIENYEJI MBARONI KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA KIJANA, UCHUNGUZI WAENDELEA WATATU MBARONI

Watu watatu akiwemo mganga wa kienyeji ambaye jina lake halijatambulika wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Singida wakituhumiwa kwa mauaji ya kijana aliyefahamika kwa jina moja la Samwaja pamoja na kumnyofoa baadhi ya viungo vya mwili kisha kuufukia mwili wa kijana huyo katika makazi yake
Tukio hilo limetokea katika kijiji na kata ya Makuro tarafa ya Mtinko mkoani Singida baada ya ndugu wa kijana huyo na wananchi wa kata hiyo kumtafuta baada ya kupotea toka tarehe 8 August 2024 alipokwenda kuangalia mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga mchezo wa ngao ya jamii

Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya wananchi wamesema walianza kumtilia shaka mganga huyo ambaye amehamia katika kijiji hicho hivi karibuni kutokana na matukio ya kuchinja mbuzi na ng’ombe wa watu katika kijiji hicho licha ya wananchi hao kuripoti matukio hayo kwa viongozi

Wananchi wa kata hiyo wanaeleza kuwa kuna watu 3 ambao wamepotea katika mazingira ya kutatanisha katika kata hiyo ambao bado hawajapatikana mpaka sasa

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Singida Godwin Gondwe amekiri kutokea kwa tukio hilo na kueleza hatua ambazo zimechukuliwa na serikali mara baada ya kutokea tukio hilo

Post a Comment

Previous Post Next Post