MIILI MINGINE MIWILI YAFUKULIWA KWA MGANGA, ULINZI WAIMARISHWA

Singida.Mara baada ya kuzuka kwa taharuki ya miili mingine kufukuliwa katika nyumba ya mganga wa Kienyeji mkoani Singida, Jeshi la polisi mkoani humo limeimarisha ulinzi katika eneo hilo huku miili hio ikifikia mitatu mpaka sasa 
Hayo yamebainishwa na kamanda wa polisi mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Amon Kakwale wakati akizungumza na wananchi ambapo amesema eneo hilo litakuwa chini ya jeshi la polisi mpaka taratibu zote zitakapokamilika

Amesema miili hio mingine iliofukuliwa imeshindwa kutambulika hivyo kitakachofanyika ni kupima vinasaba vya miili hio na wale wote waliopotelewa na ndugu zao ili waweze Kutambua miili hio ni jinsia gani na imetokana na familia gani

“Tukishachukua sampuli za miili hii na ndugu ambao walipotelewa tutafanya uchunguzi wa vinasabavinavyoweza kututambulisha jinsia ya Mwili huu na Mwili huu unatoka jinsia gani, kwasasa sio rahisi kutambua , kuanzia sasa na kuendelea eneo hili litakuwa chini ya jeshi la polisi”
Aidha Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Singida Elia Digha amesema katika maeneo yao wameingia waganga wakienyeji maarufu kama lambalamba ambao hujitafutia fedha kwa njia zisizo halali 

Ameongeza kwa kusema kuwa Kulingana na hali ilivyo kuna uwezekano wa kuwa na miili zaidi ya iliopatikana mpaka sasa katika eneo hilo hivyo ameliomba jeshi la polisi kuendelea kufanya uchunguzi zaidi katika eneo hilo

“Huyu mganga sio mzaliwa wa hapa Singida kwa kabila ni msukuma lakini amekuja kuchukua akili za wanyaturu hata alipoanza kupoteza ndugu zao hawakushtuka, kwasababu inaonekana kuna miili zaidi ya hawa, waendelee kutafutwa mpaka wapatikane” 
Kwa upande wake Mkuki Stephano mkazi wa kijiji cha makulo amesema wao kama wananchi wanaumizwa na yanayotokea katika eneo lao na kusema kuwa sio mara ya kwanza kutoka hivyo wanaiomba serikali kuimarisha ulinzi kwa kujenga kituo cha polisi katika kata yao

“Serikali ipo pamoja na wananchi ila tunaomba tujengewe kituo, wananchi watakapoona kituo kimejengwa kata ya makuro na serikali imeleta askari ambao watakuja kusimamia amani katika kata yetu, wananchi tunaumia sana haya yanayoonekana katika mitandao ndio yanayotokea hapa katikata kijiji chetu” alisema

Nae Tabu Ramadhani amesema amechukizwa na kitendo kilichotokea sababu mganga huyo alipohamia katika kijiji chao amepokelewa na kaka yake aliyezaliwa nae na kwamba marakadhaa amekuwa akimfanyia ubaya

“Nimefanyiwa vibaya na huyu mtuhumiwa huyu kaka yangu aliyepekwa Singida, mke wake na Watoto wake wamekimbia nateseka mimi kwaajili ya kakayangu, ni kaka yangu tumezaliwa tumbo moja”

Kwa upande wake Husna Mosess amesema tukio hilo lina mhuzunisha sana na linaogopesha sana sababu tokea azaliwe hajawahi kushuhudia tukio kama la namna hio

Mpaka sasa ni jumla ya miili mitatu imepatikana katika nyumba hiyo ikiwa imefukiwa na mganga huyo na baadhi ya wakazi wa kijiji cha Makuro na maeneo jirani wakichukizwa na kitendo cha mganga huyo 

Mwili wa kwanza wa kijana Samwaja Raphael ulipatikana juzi August 23, 2024 mara baada ya kupotea alipoenda kuangalia mechi ya watani wa jadi na hatimaye miili mingine miwili imepatikana kwa mganga huyo aliyejulikana kwa jina la Adam Magoko

Post a Comment

Previous Post Next Post