RAIS SAMIA AFANYA MABADILIKO TENA, UMMY AWEKWA KANDO, KABUDI NDANI

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko katika baraza la mawaziri, wakutugenzi watendaji na nafasi nyingine 

Katika taarifa iliotokewa usiku wa kuamkia leo August 15 na Ikulu Mawasiliano, Rais Samia amemteua Crispin Chalamila kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), ambapo kabla ya uteuzi huu Chalamila alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais - Ikulu na kisha amemteua Dkt. Irene Isaka kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)

Miongoni mwa mabadiko aliyoyafanya kwa wakurugenzi watendaji ni kuwabadilisha vituo vya kazi Bi. JoanFaith Kataraia aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Morogoro kwenda kuwa mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Singida akibadikishana na Bw. Jeshi Godfrey Lupembe ambaye anakwendakuwa Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Morogoro 
Bi. JoanFaith Kataraia mkurugenzi mtendaji mpya wa halmashauri ya Manispaa ya Singida akitokea halmashauri ya wilaya ya Morogoro 
Aidha amemteua Salum Hamduni kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga ambaye kabla ya hapa alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na anachukua nafasi ya Prof. Siza Tumbo ambaye amerejea Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA)

Rais Dr. Samia pia amemteua Dr. Pindi Hazara Chana kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii akichukua nafasi ya Angellah Jasmine Kairuki ambaye ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais na amemteua Profesa Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria
Prof. Paramagamba KABUDI, Waziri wa Katiba na Sheria
Ameendelea kwakumteua William Vangimembe Lukuvi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) akichukua nafasi ya Jenista Joackim Mhagama ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Afya akichukua nafasi ya Ummy Mwalimu ambapo kabla ya uteuzi huu, Mhagama alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) huku Ummy Mwalimu akiwekwa Kando katika baraza hilo la mawaziri 



Post a Comment

Previous Post Next Post