Zaidi ya wakulima 60,000 wa kilimo cha Pamba wamewezeshwa kulima kilimo cha ikolojia hai kupitia mradi wa Kijani hai chini ya Shirika la Helvetas katika mikoa ya Singida na Simiyu
Akizungumza Meneja wa mradi huo Andrew Mphuru katika maonyesho ya Nanenane jijini Dodoma amebainisha ya kuwa mradi wa Kijani hai ulianza mwaka 2017 na mpaka mwaka huu umewafikia wakulima wa idadi iliyotajwa hapo juu huku wakiwa wamelenga kuwafikia wakulima laki moja ifikapo mwaka 2028 huku lengo lao likiwa nikuwaondoa wakulima kuachana na matumizi ya kemikali
“Mradi wa Kijani Hai ulianza mwaka 2017 na umefikia zaidi ya wakulima 60,000 ila lengo letu ni ifikapo 2028 tuwe tumefikia wakulima 100,000 na hekari 150,000 za pamba hai ziwe zinalimwa kwa njia ya kilimo ikolojia hai,” amesema
Kwasasa Tanzania inashika nafasi ya kwanza Afrika na nafasi ya Tano Duniani kwa kuzalisha bora na hii inachagizwa na kilimo cha pamba hai
Kwa upande wake Tawanda Mutonhori kutoka Kampuni ya Bio Sustain ya mkoani Singida amesema kilimo ikolojia hai kimeweza kuongeza kiwango cha pamba bora katika mikoa ambayo wananunua.
“Sisi tunanunua pamba iliyolimwa kwa njia ya kilimo ikolojia hai kwa wakulima zaidi ya 24,000 wa mikoa ya Singida, Simiyu, na Shinyanga, kusema kweli pamba yao ni bora na inakubalika katika soko,” amesema.
Amesema kwa mwaka wananunua tani elfu 26 hadi 36 ya pamba iliyolimwa kwa njia ya kilimo hai, huku lengo lao ni kununua tani elfu 50
Mwakilishi wa Kampuni ya Alliance Ginery ya mkoani Simiyu, Masalu Samweli alisema kwa miaka mitatu wamewezesha zaidi ya wakulima 22,000 kulima pamba kwa njia ya kilimo hai
Amesema walianza kutoa elimu kuhusu faida za kilimo ikolojia kiafya, kimazingira na utunzaji wa ardhi, jambo ambalo limepokelewa vizuri na wakulima hai
“Kwa uzoefu wangu wa miaka mitatu ya kutoa elimu kuhusu kilimo ikilojia hai, uzalishaji wa mazao yasiyo na kemikali umeongezeka, hivyo wameweza kuona faida, hasa kupunguza gharama za uzalishaji, kutunza afya ya wakulima na ardhi na kurejeresha mazingira katika maeneo wanayohudimia,” amesema..
Tags:
HABARI


