DC GONDWE ATOA MAAGIZO MAZITO, Mazito, WADAU WAFUNGUKA KUWAITA WANANCHI, MAONYESHO YA SABA MKOANI SINGIDA

 Na. Jamaldini Abuu 
Mkuu wa wilaya ya Singida mkoani Singida Godwin Gondwe wakati akitembelea mabanda yaliopo kwenye maonyesho ya 7 ya mifuko na program za kuwasaidia wananchi kiuchumi yanayofanyika mkoani Singida amewataka mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) mkoani Singida kuongeza nguvu ya wahudumu na mitambo katika viwanja vya maonyesho 

Hii ni baada ya kukuta idadi kubwa ya watu wanaosubiri huduma huku mtambo unatumika kusajilia ni mmoja na wahudumu wakiwa ni wawili na kuwataka kutoa taarifa mapema ili nguvu iongezeke kutoka ofisi zao zilizopo katika wilaya na halmashauri za mkoa huu

"NIDA hakikisheni watu wa Singida wanapata namna za NIDA, kama kuna haja ya kuongeza mitambo, kama hamna mtuambie tuna leo na tuna kesho, nataka mnifikishie changamoto hio kwenye kikao jioni ya Leo ili kesho na kesho kutwa wananchi wapatiwe huduma sijaridhishwa na idadi yenu wawili mpk wachache hamtoshi, ongezeni watu"
Mkuu wa wilaya ya Singida mkoani Singida Godwin Gondwe akitembelea mabanda mbalimbali yaliopo katika maonyesho ya 7 Kuwawezesha Wananchi Kiuchumi katika viwanja vya bombadia mkoani Singida 
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa wao kama watumishi wanakutana sana na changamoto wanayolutana nazo kwa wananchi ni malalamiko ya namba za NIDA bado hazijatolewa za kutosha

Maonyesho hayo ya Saba ya mifuko na program za kuwasaidia wananchi kiuchumi yanayofanyika mkoani Singida kwa siku 7 yalifunguliwa na Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera bunge na uratibu William Lukuvi na kuwapa fursa wajasiriamali mbalimbali kuonyesha bidhaa zao ambazo ni matokeo ya kusaidiwa kiuchumi na mifuko na program hizo

Moja ya wanufaika hao ambaye amejitokeza katika maonyesho hayo ni Clara Sanga mwenye umri wa miaka 33 lake ni Clara Sanga Mwanadada mwenye Umri wa Miaka 33 mjasiriamali mkazi wa kijichi jijini Dar es Salaam hapa anaishauri serikali kujenga vituo jumiishi vya wajasiriamali ili maonyesho kama haya yanapoisha katika mikoa mbalimbali wajasiriamali kuweza kuacha bidhaa zao kuliko kurudi nazo walikotoka na kusema kuwa jambo hilo linawapotezea wateja

"Badala ya kurudi na mizigo Dar tuache pale iwe ni 'Centre' yetu wateja wanapokuja tunawaambia, hizi bidhaa kesho kesho kutwa tukiondoka hizi bidhaa utapata labda manispaa, kwahio inakuwa ni center moja wapo inatukuza sisi kiuchumi na kuendelea kulinda wateja wetu walioko ndani ya Singida" amesema Clara

Kwa upande wake Uswege Mwakila kutoka ofisi ya ardhi wilaya ya Manyoni amewataka wananchi kujitokeza katika maonyesho hayo ili kuweza kupatiwa hati miliki za ardhi zao na kwamba utaratibu ni rahisi akishalipia hapohapoa anapatiwa hati yake

"Mpaka sasahivi toka jana ni watu 12 wameshapatiwa hati na nyingine zimeshapelekwa kwa msajili" amesema
Hii ni siku ya tatu ya maonyesho hayo ambayo yanatarajiwa kufikia kilele siku ya tarehe 14 mwezi huu huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Naibu waziri mkuu na Waziri wa nishati Dr. Dotto Biteko, na yanafanyika katika viwanja vya bombadia 


Post a Comment

Previous Post Next Post