Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida linawashikiria watuhumiwa 137 kwa makosa mbalimbali ikiwemo watuhumiwa 21 kwa makosa ya mauaji
Hayo yamebainishwa hii leo Septemba 19,2024 na kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Singida ACP Raphael Mayunga wakati akizungumza na waandishi wa habari
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Singida ACP Raphael Mayunga akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake hii leo (Picha na Jamaldini Abuu)
Mayunga amesema baadhi ya watuhumiwa wameshafikishwa mahakamani akiwemo mganga wa kienyeji Kamba Kasubi aliyetuhumiwa kwa Kuua na kufukia Miili ya watu katika kamazi yake mkoani Singida na Dodoma
"baadhi ya watuhumiwa wameshafikishwa mahakamani akiwemo Kamba Kasubi ambaye ni mganga wa kienyeji na wenzake 13 wanaotuhumiwa kwa mauaji ya watu watatu katika Kijji cha Makuro Singida na mauji ya watu saba katika Kijji cha Porobanguma, Wilaya ya Chemba Dodoma"
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa katika kesi walizofukisha mahakamani takribani washtakiwa 43 wamehukumiwa ambapo watano walihukumiwa kunyongwa hadi kufa kutokana na makosa ya mauaji na washtakiwa watatu kwenda jela maisha kwa makosa ya kubaka na kulawiti
"Washitakiwa 43 walihukumiwa baada ya Mahakama kuridhika na ushahidi uliowasilishwa kuhusiana na makosa ya jinai waliyoyatenda. Hukumu hizo ni pamoja na kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa washitakiwa watano wa makosa ya mauaji, washitakiwa wawili kwenda jela maisha kwa kulawiti, mshitakiwa mmoja alihukumiwa jela maisha kwa kosa la kubaka nawashitakiwa wengine watano wamehukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa makosa ya kubaka" alisema
