Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamaga Kabudi amezundua rasmi Kitabu Cha Historia ya Singida kilichoandikwa na Alfred Ringi katika Ukumbi Wa Aqua Vitae mkoani Singida
Katika Uzinduzi huo uliofanyika Disemba 7, 2024 na hudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali wakiongozwa na Godwin Gondwe mkuu wa wilaya ya Singida na akimwakilisha mkuu wa mkoa pamoja na wananchi mbalimbali Prof. Kabudi amewataka Watanzani kutoponda na kumsema mwandishi kwenye mapungufu ya Kitabu Hiko watakapoyaona badala yake wakaandike muendelezo wa Historia hiyo na ikibidi kumpa mrejesho mwandishi kwaajili ya Toleo la pili
Katika hatua nyingine Prof. Palamagamba Kabudi amesimikwa na machifu wa mkoa wa Singida na kupewa jina la CHIFU MUGHENYI alipokuwa mgeni rasmi katika halfa ya uzinduzi wa Kitabu cha Historia ya Singida
Ikumbukwe kuwa CHIFU MUGHENYI ni moja kati ya machifu wa mkoa wa Singida mwenye Historia kubwa wakati wa uhai wake
Waziri Kabudi amempongeza mwandishi wa Kitabu Hiko Alfred Ringi kwa kuandika Historia kamili ya Mkoa wa Singida huku akisema vitabu vingine viliishia kuandika na kuelezea sehemu ndogo ya mkoa kama makabila ya mkoa wa Singida lakini Kitabu hiki kimejumuisha Kila kitu katika Historia ya Mkoa wa Singida
NB: Asante kwa kuendendelea KUTUAMINI na KUTUFUATILIA🙏 KAJEM TV NA BLOG YETU YA KAJEMEDIA NA MITANDAO YETU YA KIJAMII ipatikanayo kama KAJEMTV. Maoni Yako ni ya msingi sana kwetu kwani KAJEM TV #Tunakuzingatia. Wasiliana nasi Sasa kupitia Namba 0626007143 na mitandao yetu ya kijamii
#kajemtv #news #Tunakuzingatia #kajem




