AREJEA BAADA YA KUISHI NJE MIAKA 20 BILA KUWASILIANA NA NDUGU

Mwanamke mmoja raia wa India aliyetambulika kwa jina la Hamida Banu aliyesafirishwa kwa ulanghai kwenda Pakistan miongo miwili iliyopita bila kuwasiliana na familia yake hatimaye amerejea nyumbani 

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha BBC Hamida amesema alilaghaiwa kwenda Pakistan baada ya kukubali kufanya kazi iliyopaswa kuwa Dubai  mwaka 2002, ambapo awali Hamida aliwahangaikia kifedha watoto wake wanne baada ya kifo cha mumewe kwa kufanya kazi ya upishi nchini Qatar, Dubai na Saudi Arabia.
Ajuza huyo wa miaka 75 alifuatwa na wakala wa uajiri ambaye alisema atamsaidia kupata kazi huko Dubai na kumtaka Hamida alipe rupia 20,000 (dola za kimarekani 250) na badala ya Dubai, alipelekwa katika jiji la Hyderabad nchini Pakistan na alizuiliwa katika nyumba kwa miezi mitatu.

Aliiambia BBC kuwa baadaye aliolewa na mchuuzi wa barabarani huko Karachi, ambaye alikufa wakati wa janga la Covid-19 na kuwa mumewe huyo hakuwahi kumsumbua na kisa chake kilibeba vichwa vya habari mnamo Julai 2022 baada ya mwanahabari wa India, Khalfan Shaikh kutazama mahojiano ya YouTube yaliyofanywa na mwanaharakati wa mitandao ya kijamii wa Pakistani, Waliullah Maroof na kuyachapisha kwenye jukwaa lake.

Mahojiano hayo yaliifikia familia ya Bi Hamida nchini India pale mjukuu wake ambaye hakuwahi kukutana naye  alipoina video YouTube zaidi ya miezi 18 iliopita.
Bwana Shaikh na Bw Maroof wakapanga simu kati ya Bi Hamida na familia yake ya India na baada ya kufika India, Bi Hamida alikumbuka video ya 2022 ambayo ilimsaidia kuungana na familia yake baada ya miaka mingi.

NB: Asante kwa kuendendelea KUTUAMINI na KUTUFUATILIA🙏 KAJEM TV NA BLOG YETU YA KAJEMEDIA NA MITANDAO YETU YA KIJAMII ipatikanayo kama KAJEMTV. Maoni Yako ni ya msingi sana kwetu kwani KAJEM TV #Tunakuzingatia. Wasiliana nasi Sasa kupitia Namba 0626007143 na mitandao yetu ya kijamii
#kajemtv #news #Tunakuzingatia  #kajem

Post a Comment

Previous Post Next Post