Wananchi wa kata ya
Unyahati wilayani Ikungi mkoani Singida wameiomba serikali kuharakisha ujenzi
wa minara ya simu ili kurahisisha mawasiliano katika vijiji vyao kutokana na
huduma hiyo kusuasua hivyo kulazimika kupanda juu ya miti na mawe ili kupata
mawasiliano
Hayo yamejiri wakati wa ziara ya siku moja mkoani Singida
ya
Naibu waziri wa mawasiliano na teknolojia ya habari Meryprisca Mahundi ambapo
wakazi hao wa kitongoji cha Ng’ambo wamesema licha ya kuwa na simu kubwa lakini
matumizi yake ni ya simu ndogo kutokana na mtandao kutowaruhusu kuingia
mtandaoni
Nae meneja wa TTCL Mkoa wa Singida
Agustino Mwakyembe amesema wao kama TTCL
wanatekeleza ujenzi wa mnara katika kijiji cha Matale ‘A’ ambapo ujenzi
umefikia asilimia 67 huku ukikamilika unatarajiwa kutoa huduma ya 3G na 4G na
utakuwa na urefu wa mita 60
“Kwasasa ujenzi wa mnara huu umefikia asilimia 65 na unatarajiwa kufikia tarehe 31 April ujenzi utakuwa umekamilika na wananchi wa Matale na vitongoji vyake wataweza kupata huduma” alisema Mwakyembe
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Meryprisca Mahundi amewataka wamiliki na watoa huduma za mitandao nchini kukamilisha ujenzi wa mianara walioingia mikataba na wizara hiyo kabla ya tarehe 12 mwezi mei mwaka huu Hayo yamejiri wakati wa ziara yake ya siku moja mkoani singida ambapo amewataka kuharakisha na kuongeza kasi ya ujenzi ili kukamilisha kulingana na matakwa ya mkataba ili kurahisiha upatikanaji ya mtandao kwa wananchi hususani waishio vijijini
“Watoa huduma wote kufika tarehe 12 Mei muwe mumemaliza ujenzi wa minara yote na muwemumeiwasha kwamba sasa wananchi wanafurahia, wote ambao waliingia mkataba na wizara yetu ya mawasiliano wote kila mmoja ajiangalie aongeze na muda wa kufanya kazi ili kuhakikisha hii minara tunakuja kukabidhiwa na sio kuongezewa muda” alisema
NB: Asante kwa kuendendelea KUTUAMINI na KUTUFUATILIA🙏 KAJEM TV NA BLOG YETU YA KAJEMEDIA NA MITANDAO YETU YA KIJAMII
ipatikanayo kama KAJEMTV. Maoni Yako ni ya msingi sana kwetu kwani KAJEM TV #Tunakuzingatia. Wasiliana nasi Sasa kupitia
Namba 0626007143 na mitandao yetu ya kijamii #kajemtv #news #Tunakuzingatia #kajem



