Mwenge wa uhuru ulipokelewa mkoani Singida katika eneo la Sagara ukitokea mkoa wa Manyara mnano July 19, 2025 nakukimbizwa kwa takribani siku saba katika Halmashauri 7 za mkoa wa Singida kuzindua, kukagua na kuweka mawe ya msingi katika miradi hio na kutoa ujumbe wa mbio za mwaka mwaka 2025
Halmashauri ya wilaya ya Singida ndio Halmashauri ya kwanza kukimbiza Mwenge huo Siku ya Jumamosi ya July 19,2025 na kutembelea Miradi 7 ya maendeleo yenye Thamani ya takribani Bilioni 2.9
Kisha halmashauri ya wilaya ya Mkalama Ikaupokea Mwenge huo na kukimbiza siku ya Jumapili ya July 20,2025. Takribani miradi 7 ikamulikwa yenye Thamani ya takribani Bilioni 36
Halmashauri ya Tatu kukimbiza Mwenge huo ni Halmashauri ya Wilaya ya Iramba ambapo miradi 7 imemulikwa yenye Thamani ya Bilioni 7.6 na siku ya Jumatatu ya July 22 halmashauri ya Manispaa ya Singida ikaukimbiza Mwenge huo katika miradi 8 yenye Thamani ya Bilioni 7.4
Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi imekuwa ya nne katika mkoa wa singida kukimbiza mwenge wa uhuru ambapo Miradi takribani 7 imemulikwa yenye thamani ya Bil. 2.5 na baada ya mkesha mwenge ukakabidhiwa katika halmashauri ya wilaya ya manyoni
Wilaya ya Manyoni yenye Halmashauri 2 imeukimbiza mwenge huo siku mbili mtawalia ambapo katika siku ya kwanza ya Tar. 24 July ulikimbizwa katika miradi 7 yenye thamani takriban Bil. 3.5 na kuukabidhi katika halmashauri ya wilaya ya Itigi
Halmashauri ya Itigi imekuwa halmashauri ya mwisho kati ya halmashauri 7 za mkoa wa Singida kuukimbiza mwenge wa uhuru na kumulika miradi 7 yenye thamani ya Bil. 1.9
Licha ya mapokezi ya wananchi wengi wa mkoa wa Singida kujitokeza barabarani na maeneo ya miradi kuushangilia mwenge huo, imeshuhudiwa miradi mingi kuwa ya kijamii yenye nia ya kupunguza adha kwa wananchi juu ya upatikanaji wa huduma za kijamii
Miradi ambayo kwa asilimia kubwa imezinduliwa, Kukaguliwa na Mawe ya Msingi ni miradi ya Maji, Shule, Barabara, Vikundi vya vijana walionufaika na mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri, Miradi ya huduma za afya (Zahanati, Vituo vya Afya), pamoja na programu za Lishe, pambano dhidi ya dawa za kulevya, mapambano dhidi ya Rushwa pamoja na upandaji Miti kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
Hii leo July 26 mkuu wa mkoa wa Singida Mh. Halima Dendego ameukabidhi mwenge huo kwa mkuu wa mkoa wa Tabora Paul Chacha ili kuweza kuendeleza mbio za mwenge wa Uhuru katika mkoa huo
Miongoni mwa Jumbe zilizobebwa zilizobebwa na Mwenge wa Uhuru mwaka huu ni "Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 Kwa Amani Na Utulivu", "Kupambana na Rushwa ni Jukumu Langu na Lako", "Lishe Bora ni Msingi wa Afya Imara Zingatia Unachkula"






.jpg)
.jpg)
