Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Singida Sipha Mwanjala akizungumza na waandishi wa habari amebainisha uwepo wa baadhi ya watumishi mkoani humo kufikishwa mahakamani kutokana na matumizi mabaya ya madaraka na kughushi nyaraka
Hayo ameyabainisha Julai 26,2024 akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema watumishi hao takribani watano wameshafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika
Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Singida Sipha Mwanjala kulia akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya watumishi watano kufikishwa mahakamani "Tumefanya uchunguzi na uchunguzi ulipokamilika wakafikishwa mahakamani ila ni kweli wapo watumishi ofisi ya mkuu wa mkoa wamefikishwa mahakamani kwa matumizi mabaya ya mamlaka, kughushi" alisema Mwanjala
Mwanjala amesema katika kipindi cha miezi 3 wameokoa zaidi ya sh136 milioni fedha zilizotokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo
Amesema katika fedha hizo, zaidi ya sh18 milioni na laki nane zimeokolewa katika halmashauri ya Mkalama na zaidi ya sh1 milioni na laki tisa zikiokolewa na katika halmashauri ya Itigi huku zaidi ya sh1 milioni na laki moja ziliokolewa katika halmashauri ya Iramba
Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Singida Sipha Mwanjala kulia akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya watumishi watano kufikishwa mahakamani
Aidha ameongeza kuwa wamepokea malalamiko 55 huku malalamiko 20 yakihusu vitendo vya rushwa na malalamiko 35 hayakuhusu malalamiko ya rushwa huku uchunguzi ukiendelea katika malalamiko hayo yaliohusiana na rushwa
"Kesi 3 zilifunguliwa mahakani, kesi 5 ziliamuliwa kati ya hizo kesi 4 jamhuri ilishinda ikiwemo kesi iliotokana na maagizo ya waziri mkuu aliyoyatoa alipofanya ziara katika wilaya ya Manyoni na kesi moja ilishindwa" alisema
Mwanjala amewataka watendaji wote wa halmashauri hasa kitengo cha manunuzi kutumia mfumo wa manunuzi wa NEST ili kuzuia mianya ya rushwa
Tags:
HABARI


Tupe Maoni Yako Kuhusu Kuboresha Habari Zetu Ili Tukufikie Kwa Kadiri Unavyotamani Kwani Sisi Tunasema. #NiSisinaWewe
ReplyDelete