Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeandaa mafunzo maalumu kwa Mtandao wa Mabloga (TBN) kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. Mafunzo haya yatafanyika Leo Jumatatu, Agosti 11, 2025, katika Makao Makuu ya TCRA
Kwa mujibu wa taarifa kutoka TCRA mafunzo hayo yana lengo la kuwaandaa mabloga na wanahabari kwa ujumla ili waweze kuripoti habari za uchaguzi kwa weledi na uadilifu
Baadhi ya mada zitakazojadiliwa ni pamoja na Mwongozo wa Waandishi wa Habari katika Uandishi wa Habari za Uchaguzi, Kanuni za Utangazaji wa Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa za Mwaka 2020, na uhusiano kati ya Waandishi wa Habari na Jeshi la Polisi katika kulinda usalama
Mada nyingi zitatoka Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari, itakayozungumzia maadili na sheria kwa waandishi wa habari, mada kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii na Akili Mnemba (AI) kuelekea uchaguzi na mada kutoka Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) itakayozungumzia Ulinzi wa Taarifa Binafsi kuelekea uchaguzi
Mafunzo haya yanatarajiwa kuwa na faida kubwa kwa mabloga na jamii kwa ujumla kwani yatawawezesha wanahabari kutoa taarifa sahihi na zenye uwajibikaji, jambo ambalo ni muhimu katika kujenga mazingira ya uchaguzi yenye amani na utulivu
Pia, yanatoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii na Akili Bandia ili kuepuka taarifa za uongo.

