Zaidi ya Shilingi Milioni 100 kutoka Serikalini zimetumika kama ruzuku ya Nishati safi ya kupikia katika halmashauri ya wilaya ya Singida mkoani humo huku majiko banifu takribani 1,115 ya ruzuku yakitarajiwa kugawiwa kwa awamu ya kwanza wilayani humo
Hayo ameyasema Mkuu wa wilaya ya Singida Godwin Gondwe wakati akigawa mitungi 500 ya Gesi katika kata ya Itaja na kutoa maagizo ya mwezi mmoja kwa makampuni yaliyopewa dhamana kusambaza nishati hiyo kufungua mawakala wa kubadilisha Gesi inapoisha katika kila eneo ambalo Gesi hiyo inasambazwa
Maagizo hayo yamekuja kufuatia wananchi wa eneo hilo kuiomba serikali kuongeza idadi ya mitungi ya Gesi inayogawiwa kwa ruzuku kutokana na uhitaji kuwa mkubwa kwa wananchi pamoja na kufungua mawakala wa kubadilisha kutokana na umbali wa kwenda mjini
Hawa Hussein Mkazi wa Itaja ameishukuru Serikali kwa majiko hayo na kusema siku za nyuma waliyaona tu mijini na kuyatamani kisha akaiomba serikali kuongeza idadi ya majiko hayo kutokana na uhitaji kuwa mkubwa wananchi pamoja na kuweka mawakala wa kubadilisha gesi katika vijiji vyao
Wananchi hao wamesema Gesi hiyo ni kama miujiza ambayo zamani hawakufikiria kutumika katika maeneo na kusema kuwa itawaondolea usumbufu wa kutafuta kuni na ukataji miti uliokithiri kutokana na uchomaji mkaa ambapo mitungi hiyo iliyogawiwa inafikisha idadi ya mitungi takriban 3796 ilikwisha gawiwa mpaka sasa katika wilaya hiyo
Tags:
HABARI






