TAKUKURU SINGIDA YAREJESHA ZAIDI YA MILIONI 167 SERIKALINI KUPITIA UTEKELEZAJI WAO

Taasisi ya Kuzuia na Kupambanua na Rushwa TAKUKURU mkoa wa Singida imefanikiwa kuoka na kurejesha serikalini zaidi ya milioni 167 kupitia ufuatiliaji wa matumizi ya Fedha za utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya maendeleo, Uchunguzi na Mashta.

Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Singida SOSTHENES KIBWENGO amesema hayo wakati akitoa taarifa yake ya kipindi cha Januari hadi Machi 2026 kwa waandishi wa habari.

KIBWENGO alisema kati ya fedha hizo zaidi ya Milioni 56 zimerejeshwa kupitia ufuatiliagaji wa ukusaji wa Mapato kwa njia ya mashine za kielektroniki za 'POS' katika halmashauri za Manyoni na Iramba, baada ya kubainika kuwa Fedha hizo hazikuwasilisha Benki kwa wakati kama ilivyotakiwa kwa mjibu wa taratibu za ukusanyaji wa mapato ya umma.

Alisema katika kipindi hicho cha Januari hadi Machi mwaka huu zaidi ya Milioni 76 zimerejeshwa kutokana na ufuatiliaji wa matumizi ya Fedha za utekelezaji wa Miradi ya maendeleo 28 yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 8 katika sekta ya Elimu, Afya, Barabara, Utawala na Maji.
Aidha KIBWENGO alisema kuhusu Uchunguzi na Mashta zaidi ya Milioni 34 zimerejeshwa serikalini kutokana na chunguzi za tuhuma mbalimbali za ubadhirifu wa mali za umma, huku malalamiko 95 yalipokelewa, kati ya hayo 51 yalihusu vitendo vya Rushwa na 44 hayakuhusu vitendo vya Rushwa ambapo wahusika walishauriwa ipasavyo.

Katika kipindi hicho pia mashauri 6 yalifunguliwa mahakamani, mashauri 3 yalitolewa uamuzi mahakamani na Jamhuri imeshinda mashauri yote 3.

KIBWENGO pia alitoa wito kwa wananchi kuendelea kushiriki katika mapambano dhidi ya rushwa kwa kutoa taarifa za vitendo vya Rushwa.

Katika kipindi cha Aprili hadi Juni 2026 TAKUKURU imejipanga kuendelea kuimarisha uzuiaji wa vitendo vya rushwa kwa kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa Miradi ya maendeleo pamoja na kuendelea kutoa elimu kwa umma kwa kuwafikia na kushirikiana na makundi mbalimbali ya wadau ili kujenga usawa na tabia ya kuchukia Rushwa.


Post a Comment

Previous Post Next Post